NIKIPEWA NAPENDELEWA?
Nineshindwa kujuwa,ni kipi kinachokuchoma
Mambo yangu sawasawa,zamu yako kunisema
Nduguyo ‘mefanikiwa,kwako wewe ni husuma
Ukipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa?
Nineshindwa kujuwa,ni kipi kinachokuchoma
Mambo yangu sawasawa,zamu yako kunisema
Nduguyo ‘mefanikiwa,kwako wewe ni husuma
Ukipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa?
Mwenzangu wanidhihaki,kwa yale wanitendea
Tangu jadi una chuki,kisasi waniwekea
Utendayo sio haki,laana wajiletea
Ukipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa?
Niliposhinda mchezo,tuzo nyingi nilipewa
Ulitilia mkazo,kwamba nilipendelewa
Uliibua mizozo,mpaka ukatimuliwa
Ukipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa?
Ulijawa na kinyongo,mengi ‘kanizingizia
Ulisema mimi chongo,polisi nikafelia
Nikatunga zangu tungo,kaniita haramia
Ukipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa?
N‘kaomba usaidzi,hali ilipogeuka
Ulisema mimi mwizi,hamna yalonifika
Nikajua we‘ chizi,makuu yatakufika
Ukipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa?
Kisasi sitalipiza,mema nitakuombea
Daima nitajikaza,Mola atanitetea
Chozi atanipanguza,kileleni ntapepea
Ulipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa?
Malenga nashuka ngazi,kurasa nazifunika
Namaliza yangu kazi,pande zote nasikika
Nimesema waziwazi,sio kwamba napayuka
Ukipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa??
UTUNZI WA Jicho La Pembeni Na Malenga Wa Nchi Kavu©2015
Bahari ya Maonevu
Tangu jadi una chuki,kisasi waniwekea
Utendayo sio haki,laana wajiletea
Ukipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa?
Niliposhinda mchezo,tuzo nyingi nilipewa
Ulitilia mkazo,kwamba nilipendelewa
Uliibua mizozo,mpaka ukatimuliwa
Ukipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa?
Ulijawa na kinyongo,mengi ‘kanizingizia
Ulisema mimi chongo,polisi nikafelia
Nikatunga zangu tungo,kaniita haramia
Ukipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa?
N‘kaomba usaidzi,hali ilipogeuka
Ulisema mimi mwizi,hamna yalonifika
Nikajua we‘ chizi,makuu yatakufika
Ukipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa?
Kisasi sitalipiza,mema nitakuombea
Daima nitajikaza,Mola atanitetea
Chozi atanipanguza,kileleni ntapepea
Ulipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa?
Malenga nashuka ngazi,kurasa nazifunika
Namaliza yangu kazi,pande zote nasikika
Nimesema waziwazi,sio kwamba napayuka
Ukipewa wastahili,n‘kipewa napendelewa??
UTUNZI WA Jicho La Pembeni Na Malenga Wa Nchi Kavu©2015
Bahari ya Maonevu
No comments:
Post a Comment