Kuna kosa twalifanya, maelezo tukitoa
Watanzania na Wakenya, naomba kuwakosoa
Ndugu yenu nawakanya, umoja sitabomoa
Na urefu wa kunguni, unafika mita ngapi?
Watanzania na Wakenya, naomba kuwakosoa
Ndugu yenu nawakanya, umoja sitabomoa
Na urefu wa kunguni, unafika mita ngapi?
Mgeni akitokea, apatane na mwenyeji
Pengine amepotea, tariki ‘kienda jiji
Dira anayopokea, ni yale hayahitaji
Na urefu wa kunguni, unafika mita ngapi?
Pengine amepotea, tariki ‘kienda jiji
Dira anayopokea, ni yale hayahitaji
Na urefu wa kunguni, unafika mita ngapi?
Sio babu sio bibi,ndo‘ ndimi zasheheni
Na hawa washababi,vilevile waighani
Dodoma na Nairobi,ni urefu wa kunguni??
Na urefu wa kunguni,unafika mita ngapi?
Na hawa washababi,vilevile waighani
Dodoma na Nairobi,ni urefu wa kunguni??
Na urefu wa kunguni,unafika mita ngapi?
Kilomita mia moja, hata huo wa kunguni??
Hiki nacho ni kioja, mna matani jameni
Eleza moja kwa moja, ‘sitiane matatani
Na urefu wa kunguni, unafika mita ngapi?
Hiki nacho ni kioja, mna matani jameni
Eleza moja kwa moja, ‘sitiane matatani
Na urefu wa kunguni, unafika mita ngapi?
N‘kafika Mariakani, njiani kwenda Kilifi
Nikashuka Msufini, kusalimu wangu wifi
Nile‘lezwa kwa kunguni, kulivyo na mali ghafi
Na urefu wa kunguni, unafika mita ngapi?
Nikashuka Msufini, kusalimu wangu wifi
Nile‘lezwa kwa kunguni, kulivyo na mali ghafi
Na urefu wa kunguni, unafika mita ngapi?
Mtoapo maelezo, tumia lugha nadhari
Lugha wazi huwa nguzo, hususa kwenye safari
Ba‘adhi ya semi hizo, za‘eza leta hatari
Na urefu wa kunguni, unafika mita ngapi?
Tamati mwanaisimu, wosia nimemaliza
Nimeshapunguza sumu, na nyoyo nimetuliza
Kumbuka mimi nwalimu, Kiswahili natukuza
Na urefu wa kunguni, unafika mita ngapi????
UTUNZI WA Jicho La Pembeni Na Malenga Wa Nchi Kavu©2015
No comments:
Post a Comment